Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa Rais wa Yanga na Mwenyekiti wa umoja wa klabu barani Afrika Injinia Hersi Said.
Kwa msimu mitano mfululizo, Hersi amechora na kuongoza dira ya mafanikio ya Yanga. Zaidi ya mataji 15 yametua Jangwani.
Akiwa ukiongoni mwa kipindi chake cha kwanza cha miaka minne ya uongozi wake, Hersi amewapa kila sababu Wanachama wa Yanga kumchagua kwa awamu nyingine ya miaka minne katika uchaguzi utakaofanyika wiki ijao.
Hersi anatetea kiti chake akiwa hana mpinzani, hii ni kuonyesha kwa kiasi gani Wananchi wana imani kubwa kwa uongozi wake.
Tunamtakia kila la kheri katika siku hii ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
HAPPY BIRTHDAY HERSI...!
ADVERTISE HERE