Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wamefikia makubaliano na klabu ya Chippa United kwa ajili ya mauziano ya mshambuliaji wa Kimataifa wa Eswatini Justice Figuareido (27).
Yanga imenunua mkataba wa mwaka mmoja ambao mshambuliaji huyo alikuwa amesalia nao kuwatumikia Chippa United msimu ujao.
Yanga imepewa ruhusa ya kumalizana na Figuareido upande wa masuala ya maslahi binafsi ya mchezaji ambapo inaelezwa tayari mazungumzo hayo yalishafanyika kitambo.
Figuareido anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga akitarajiwa kuwasili nchini hivi karibuni kuungana na mabingwa hao wa nchi walioanza maandalizi ya msimu mpya Avic Town.
Ni suala la muda tu Yanga itatambulisha usajili wa mshambuliaji huyo aliyehusika kwenye mabao 7 ligi kuu ya Afrika Kusini msimu uliopita.