Masalanga, Sure Boy wapo sana Jangwani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jul 2026
Masalanga, Sure Boy wapo sana Jangwani

Jana kulikuwa na zoezi la kufanyiwa vipimo vya afya kwa wachezaji wa Yanga kabla ya kuingia rasmi kambini kuanza maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2026/27.

Kilichowafurahisha Wananchi ni kuwashuhudia baadhi ya nyota ambao kulikuwa na hatihati huenda wasiwe sehemu ya kikosi cha mabingwa hao wa nchi msimu ujao.

Kiungo mkongwe, mwandamizi Salum Abubakar 'Sure Boy' ni miongoni mwa wachezaji ambao walishiriki zoezi hilo.

Imeelezwa kuwa Sure Boy maarufu 'Babu Kaju' ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa soka Tanzania Bara.

Yanga imeamua kumbakisha Sure Boy kutokana na uzoefu wake lakini pia ni mchezaji muhimu linapokuja suala la uhamasishaji kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Katika zoezi hilo pia alionekana mlinda lango Hussein Masalanga ambaye mkataba wake wa mkopo kutoka klabu ya Singida BS ulimalizika mwishoni mwa msimu uliopita.

Yanga imemsajili Masalanga moja kwa moja akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Singida BS kufika tamati. Masalanga nae amesaini mkataba wa mwaka mmoja.

Lakini pia winga Denis Nkane ambaye msimu uliopita aliitumikia TRA United kwa mkopo, amerejea kikosini.

Kutokana na ugumu wa ratiba msimu huu Yanga inatarajiwa kuwa na kikosi chenye wachezaji kati ya 35 na 40.

Hivi karibuni Rais wa TFF Wallace Karia alizishauri klabu kusajili wachezaji wengi ili kwendana na mikiki mikiki ya ratiba ngumu ya mechi msimu ujao.

Ligi Kuu ya NBC inapaswa kumalizika mwezi May ili kupisha maandalizi ya michuano ya Afcon 2027 itakayoanza katikati ya mwezi Juni 2027.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’