Baada ya mapumziko takribani wiki tatu, wachezaji wa Yanga leo wanarejea mazoezini kuanza maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2026/27.
Yanga itaweka kambi yake Avic Town chini ya benchi jipya la ufundi linaloongozwa na kocha mkuu Manqoba Mngqithi.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema kabla ya kuanza rasmi program za mazoezi, kutakuwa na zoezi la wachezaji kupima afya.
Baadhi ya nyota wapya ambao usajli wao umekamilika wanatarajiwa kuanza rasmi kuonekana machoni kwa Wananchi.
Yanga tayari imeanza kuwatambulisha nyota hao ambapo zoezi hilo la utambulisho linatarajiwa kuendelea leo.
ADVERTISE HERE