Inaelezwa Yanga inapambana kumshawishi kiungo wa timu yaa Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Alphonce Mabula ajiunge na mabingwa hao wa soka Tanzania Bara.
Mabula yuko nchini kwa mapumziko huku akijipanga upya baada ya kumaliza mkataba kunako klabu ya Shamakhi ya Azerbaijani.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 bado ana malengo ya kurejea Ulaya kuendeleza soka lake lakini inaelezwa mabosi wa Yanga wamemuwekea mezani ofa kubwa inayoweza kumshawishi ajiunge na miamba hao wa soka Tanzania.
Mabula amecheza Ulaya kwa takribani misimu minne ambapo kabla ya kutua Shamakhi Januari 2025, alikuwa mchezaji wa Spartak Subotica ya Serbia aliyoanza kuitumikia Februari 2022, alipojiunga nayo akitokea kikosi cha Alliance FC. Pia amecheza RFK Novi Sad msimu wa 2024-2025 kwa mkopo.
Mabula anayemudu vyema kucheza nafasi zote za kiungo, ni miongoni mwa wachezaji tegemeo kwenye kikosi cha Taifa Stars akiitwa kwa mara ya kwanza Mei 30, 2025 chini ya kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’.