Yanga yasajili wawili Mashujaa Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jul 2026
Yanga yasajili wawili Mashujaa Fc

Mabosi wa Yanga wanaendelea na maboresho ya kikosi kwa usiri mkubwa jana wakimtangaza Manqoba Mngqithi, kuwa kocha mkuu akichukua mikoba iliyoachwa na Pedro Goncalves ambaye nae juzi amejiunga na AS FAR ya Morocco.

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga imedokeza kuwa maboresho yanaendelea ambapo klabu hiyo iko kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa walinzi wawili kutoka klabu ya Mashujaa Fc.

Ndio! Yanga imetua mkoani Kigoma kuibomoa Mashujaa Fc wakikamilisha michakato ya usajili wa beki wa kati Mohamed Mussa na mlinzi wa kulia Abdulnasir Gamal.

Gamal anatua kuchukua nafasi ya Israel Mwenda ambaye mkataba wake na Wananchi umemalizika wakati usajili wa Mohamed Mussa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha eneo la mabeki wa kati.

Msimu ujao ukuta wa Yanga hasa mabeki wa kati wote watakuwa wachezaji wa ndani. Mussa na Nasri Kombo wakiongezwa kuungana na Ibrahim Bacca, Dickson Job na Bakari Mwamnyeto.

Juzi wakati kalenda ya msimu mpya inatangazwa, Rais wa TFF Wallace Karia alitoa tahadhari kwa klabu kusajili wachezaji wengi ili kuwa na vikosi vipana kukabiliana na ratiba ya msimu ujao.

Ligi Kuu 2026/27 inapaswa kumalizika Mwezi Mei hivyo ni wazi kutakuwa na vipindi vya kucheza mechi 'bandika bandua'.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’