Goncalves mbioni kutua AS FAR

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jul 2026
Goncalves mbioni kutua AS FAR

Kocha wa zamani wa Yanga Pedro Goncalves yuko kwenye mazungumzo na klabu ya AS FAR kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

AS FAR wameachana na aliyekuwa kocha wao mkuu Alexandre Santos kufuatia timu hiyo kushindwa kufuzu kwa michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao wakimaliza nafasi ya nne ligi kuu ya Morocco.

Goncalves hakuwa na timu tangu alipofutwa kazi na Yanga May 06 mwaka huu. Uongozi wa klabu ya Yanga ulimfuta kazi Goncalves muda mfupi baada ya timu hiyo kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC FC katika Uwanja wa KMC Complex.

Kufuatia maamuzi hayo, benchi la ufundi lilikabidhiwa kwa Abdihamid Moalin na Patrick Mabedi kukaimu nafasi hizo hadi mwisho wa msimu wakifanikiwa kutetea taji la ligi kuu.

Kocha huyo raia wa Ureno, aliiongoza Yanga kwa sehemu ya kubwa ya msimu akichukua mikoba iliyoachwa na Romain Folz ambaye nae alifutwa kazi mwanzoni mwa msimu.

Yanga na AS FAR zilikuwa kundi B kwenye hatua ya makundi ligi ya mabingwa msimu uliomalizika AS FAR wakipoteza mchezo dhidi ya Yanga Zanzibar na wao kushinda Morocco. Waliweza kufuzu hatua ya robo na kusonga mbele mpaka fainali ambapo walifungwa na Mamelodi Sundowns.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12m ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’