Yanga kutoshiriki Kagame Cup, kuweka nguvu kwenye pre-season

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jul 2026
Yanga kutoshiriki Kagame Cup, kuweka nguvu kwenye pre-season

Wakati michuano ya kombe la Kagame ikitarajiwa kuanza kutimua vumbi Julai 24, Yanga haitashiriki michuano hiyo itakayofanyika nchini Rwanda.

Droo ya michuano hiyo inatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa, Julai 10 huku klabu za Singida BS na Simba za Tanzania Bara zikithibitisha kushiriki na KVZ ya Zanzibar nayo ikithibitisha ushiriki wake.

Yanga ambao ni mabingwa wa Tanzania Bara kwa misimu mitano mfululizo walipokea mwaliko rasmi lakini kutokana na mipango yao, wamechagua kutoshiriki.

Wakati Yanga ikihitimisha shamrashamra za ubingwa wa sita, Rais wa klabu hiyo Injinia Hersi Said alidokeza kuhusu maandalizi kuelekea msimu ujao wa mashindano 2026/27.

Hersi alisema tayari wana mialiko kutoka nchi mbili tofauti zilizoandaa michuano maalum ya pre-season. Lakini pia alisema Yanga inaweza kushiriki michuano mingine ya pre-season ambayo inaweza kufanyika visiwani Zanzibar.

Uongozi wa Yanga bado haujaweka wazi ratiba ya pre-season kuelekea msimu ujao kwa sasa wakiwa kwenye mchakato wa mabpresho ya benchi la ufundi wakitarajiwa kumtangaza kocha mkuu hivi karibuni.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’