Yanga yamnyemelea kiungo fundi Uganda, Okello ahusika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Jul 2026
Yanga yamnyemelea kiungo fundi Uganda, Okello ahusika

Tetesi kutoka duru za usajili, zimebainisha kuwa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga wako kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo mahiri wa Uganda Bobosi Byaruhanga anayeichezea klabu ya Oakland Roots kutoka jiji la California nchini Marekani.

Misimu miwili iliyopita Yanga ilijaribu kumnasa Bobos wakati huo akiitumikia timu ya Vipers Fc hata hivyo ofa kutoka Marekani ilimshawishi zaidi. Inaelezwa wakati huu kiungo mshambuliaji wa Yanga Allan Okello anahusika katika mpango wa kumshawishi Bobos atue kwa Wananchi.

Taarifa kutoka Uganda ikidokezwa na mmoja wa mastaa wanaoichezea Vipers Fc, amebainisha kuwa Bobos amewasiliana na Okello akitaka taarifa zaidi kuhusu maisha ya hapa Tanzania ndani ya klabu ya Yanga.

“Bobosi anaweza kuja Yanga , nimeona anawasiliana na Allan (Okello) akimuuliza namna maisha ya Yanga yalivyo, ametafutwa na viongozi wa Yanga wanataka kumchukua lakini bado hawajamalizana mpaka sasa, alisema mmoja wa mastaa wa Vipers ambaye pia ni rafiki wa Okello.

“Nimemuuliza anasema mazungumzo yao yanakwenda vizuri na yeye Allan amemwambia vizuri kwamba maisha ni mazuri tu hapo Yanga amepokelewa vizuri, wanalipa vizuri na viongozi na mashabiki wanaishi vizuri na wachezaji wao." staa huyo alinukuliwa na Mwanaspoti

Msimu wa 2024/25 Bobos alitikisha tetesi za usajili nchini akihusishwa na vigogo wa soka klabu za Yanga na Simba lakini aliamua kutimkia Marekani.

Hata hivyo kiungo huyo kwa sasa anaonekana yuko tayari kurejea tena Afrika kuendeleza soka lake baada ya mambo kutoenda kama alivyotarajia huko Marekani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
14h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
23h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’