Fadlu, Yanga mazungumzo yamevunjika, msako wa kocha mpya unaendelea

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Jul 2026
Fadlu, Yanga mazungumzo yamevunjika, msako wa kocha mpya unaendelea

Uongozi wa Yanga unaendelea na mchakato wa kumpata kocha mpya atakayechukua mikoba iliyoachwa na Pedro Goncalves, imefahamika.

Awali kulikuwa na taarifa mabingwa hao wa soka Tanzania bara kuwa kwenye mazungumzo na kocha wa zamani wa Raja CA Fadlu Davids lakini inaelezwa mzungumzo hayo yamevunjika.

Kwa mujibu wa mchambuzi na mwandishi wa habari za michezo wa Afrika Kusini Ayabonga Mthembu, pande mbili hazikufikia makubaliano kwenye masuala ya bonasi.

Yanga sasa inaendelea na mchakato wa kumsaka mrithi wa Pedlo ambapo pengine mpaka kufikia mwishoni mwa wiki hii huenda akafahamika.

Aidha bado Yanga haijatangaza kulivunja benchi lake la muda lililoongozwa na kocha Abdihamid Moalin na Patrick Mabedi makocha hao nao wakisikilizia hatma zao kuelekea msimu ujao.

Moalin na Mabedi ameiongoza Yanga kwenye mechi 7 za mwishoni mwa msimu wakipoteza michezo miwili mmoja wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji na mwingine wa kombe la CRDB nusu fainali dhidi ya Azam Fc.

Hata hivyo waliweza kutimiza malengo ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’