Kalenda ya mashindano ya CAF 2026/27 hadharani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Jul 2026
Kalenda ya mashindano ya CAF 2026/27 hadharani

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetangaza rasmi kalenda ya mashindano ya CAF Champions League pamoja na Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup) kwa msimu wa 2026/27,  ratiba ikianza mapema Septemba 2026.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mashindano yataanza rasmi kati ya tarehe 4 hadi 6 Septemba 2026, kabla ya kuendelea kwa michezo ya marudiano wiki moja baadaye.


HATUA YA AWALI (PRELIMINARY ROUND)

Michuano ya awali itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini:

  • Mechi za kwanza: 4–6 Septemba 2026

  • Mechi za marudiano: 11–13 Septemba 2026

Hatua hii itaamua timu zitakazoingia kwenye raundi inayofuata ya mashindano.


RAUNDI YA PILI

Raundi ya pili, ambayo mara nyingi huamua hatma ya klabu nyingi za Afrika Mashariki na Kaskazini, itachezwa mwezi Oktoba:

  • Mechi za kwanza: 16–18 Oktoba 2026

  • Mechi za marudiano: 23–25 Oktoba 2026

Hapa ndipo presha huongezeka kwa klabu zinazotafuta kufuzu hatua ya makundi.


HATUA YA MAKUNDI (GROUP STAGE)

Hatua ya makundi, inayohusisha vigogo wa soka Afrika, itaanza Novemba 2026 hadi Januari 2027:

  • Mechi ya 1: 27–29 Novemba 2026

  • Mechi ya 2: 4–6 Desemba 2026

  • Mechi ya 3: 18–20 Desemba 2026

  • Mechi ya 4: 8–10 Januari 2027

  • Mechi ya 5: 15–17 Januari 2027

  • Mechi ya 6: 22–24 Januari 2027

Hatua hii ndiyo huamua nani anaenda hatua ya mtoano, na nani anaaga mashindano.


HATUA YA MTOANO (KNOCKOUT STAGE)

Robo Fainali

  • Mechi za kwanza: 26–28 Februari 2027

  • Mechi za marudiano: 5–7 Machi 2027

Nusu Fainali

  • Mechi za kwanza: 9–11 Aprili 2027

  • Mechi za marudiano: 16–18 Aprili 2027

Hapa ndipo ubora wa kikosi, uzoefu na kina cha benchi huanza kuamua hatma ya ubingwa.


FAINALI

Fainali ya CAF 2026/27 itachezwa kati ya:

  • 9–31 Mei 2027

CAF bado itathibitisha mfumo wa fainali (mkondo mmoja au miwili) pamoja na uwanja mwenyeji.


Yanga, mabingwa wa soka Tanzania Bara 2025/26 na watani zao Simba watashiriki michuano ya ligi ya mabingwa huku Azam Fc na Singida BS wakishiriki kombe la Shirikisho (CAFCC)

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’