Goncalves apongeza ubingwa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Jun 2026
Goncalves apongeza ubingwa Yanga

Kocha wa zamani wa Yanga SC, Pedro Gonçalves, ameipongeza klabu hiyo kufuatia mafanikio ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa tano mfululizo, mafanikio yanayoendelea kuonyesha ubabe wa Wananchi katika soka la Tanzania.

Pedro, ambaye alihusika kwa sehemu kubwa katika safari ya ubingwa kabla ya kuondoka klabuni hapo mwezi Mei na nafasi yake kuchukuliwa na Abdihamid Moalin, amesema aliona dalili za ubingwa mapema baada ya Yanga kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba SC.

Kwa mujibu wake, matokeo hayo ya dabi yalikuwa ishara muhimu kwamba Yanga ilikuwa tayari imefungua njia ya kutetea ubingwa wao.

Akiandika kwa hisia, Pedro alisema:

“Tulipopata sare ngumu ugenini kwenye uwanja wa wapinzani wetu wakuu tarehe 3 Mei, tukifanya comeback ya kuvutia katika mchezo huo tukiwa tayari tunaongoza kwa pointi tano pamoja na faida ya matokeo ya head-to-head, sote tulijua kwamba ingawa bado kulikuwa na safari ya kumaliza msimu, jambo moja lilikuwa la uhakika… Yanga Bingwa!!!”

Goncalves aliongeza kuwa baada ya matokeo hayo, aliamini kabisa kuwa kilichobaki kilikuwa ni kumaliza msimu kwa nidhamu, umakini na uthabiti, jambo ambalo Yanga imefanikiwa kulitekeleza hadi kutwaa ubingwa.

Pia aliwapongeza Wananchi kwa mshikamano wao mkubwa pamoja na benchi la ufundi lililoendelea kuisimamia timu hadi kufanikisha malengo ya msimu.

“Hongereni Wananchi!!” alihitimisha ujumbe wake.

Goncalves aliingoza Yanga kutwaa taji la Mapinduzi mapema mwaka huu na hivyo kufanya Wananchi wamalize msimu na mataji matatu wakiwa pia ni mabingwa wa Ngao ya Jamii.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’