Tunajua mechi itakuwa ngumu, tutapambana tupate ushindi - Mshery

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Jun 2026
Tunajua mechi itakuwa ngumu, tutapambana tupate ushindi - Mshery

Mlinda lango wa Yanga Aboutwalib Mshery amewaalika mashabiki uwanja wa KMC Complex kuwaunga mkono kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya TRA United ambao utapigwa kesho Jumamosi Juni 27.

Ukiwa ni mchezo wa raundi ya 29, ushindi utaiweka Yanga karibu na ubingwa wa tano mfululizo kwani kama watashinda kesho huenda wakahitaji angalau alama moja tu kwenye mchezo wa kuhitimisha msimu dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa Jumanne ijayo.

Mshery amesema wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu lakini ameahidi watakwenda kupambana kusaka ushindi huku akitaja sapoti ya mashabiki wao kama silaha muhimu.

“Mchezo wa kesho ni mgumu sana. Hakuna urahisi wowote katika mchezo huu. Tunahitaji alama tatu muhimu kujiweka sawa kwa mchezo wa mwisho wa ligi."

"Tunahitaji sana hamasa ya mashabiki wetu kuanzia mchezo wa kesho na mchezo wa mwisho. Hamasa yao itatupatia nguvu kubwa kupata matokeo mazuri,” alisema Mshery.

Yanga itashuka kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana kwenye mchezo wa mwisho walipokutana uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Hata hivyo wakati huu Yanga itashuka uwanjani ikiwa na kikosi chake kamili, matarajio ya Wananchi yakiwa kuondoka na alama zote tatu.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
15h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’