Yanga vs Azam Fc; Ni mechi kubwa, mechi ya maamuzi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jun 2026
Yanga vs Azam Fc; Ni mechi kubwa, mechi ya maamuzi

Leo ni siku nyingine muhimu katika safari ya ubingwa kwa Yanga wanaposhuka dimbani kwenye Uwanja wa New Amaan Complex kuikabili Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, mzunguko wa 28.

Ni mechi yenye hadhi ya nyota tano. Dakika 90 ambazo zinaweza kuwa na mchango mkubwa katika hatima ya mbio za ubingwa, huku Yanga ikisaka kuendelea na ndoto ya kutwaa taji la ligi kwa msimu wa tano mfululizo.

Kwa namna mazingira yalivyo hivi sasa, unaweza kusema ni Yanga dhidi ya dunia. Presha ni kubwa ndani na nje ya uwanja. Wananchi na mashabiki wa Yanga wana jukumu la kuisukuma timu yao kuelekea ushindi, wakati wengi wa wapinzani wao wakisubiri kuona mabingwa hao wakiteleza katika hatua hii muhimu ya msimu.

Kwa wachezaji wa Yanga, huu ni mtihani mwingine wa kuonyesha ubora wao. Wana dakika 90 za kuwanyamazisha wakosoaji waliotawala mijadala ya mitandaoni au kuwapa nafasi zaidi ya kuendelea kuikosoa timu hiyo.

Kitu kinachowapa matumaini Wananchi ni rekodi yao katika Uwanja wa New Amaan Complex. Huu ni uwanja ambao Yanga imeutumia mara nyingi zaidi msimu huu na imeonyesha uimara mkubwa. Katika michuano ya ligi ya mabingwa (CAFCL), Yanga imecheza hapa dhidi ya vigogo kama Al Ahly, AS FAR na JS Kabylie, huku Al Ahly pekee akifanikiwa kuondoka na sare.

Ndiyo maana mchezo wa leo dhidi ya Azam FC unaweza kuwekwa katika kiwango hicho cha mechi kubwa. Tofauti pekee ni kwamba safari hii Yanga haitafuti matokeo mawili kati ya matatu. Inahitaji matokeo ya aina moja tu, ushindi.

Kumbukumbu za siku tatu zilizopita bado ni mbichi. Azam FC iliiondoa Yanga katika Kombe la CRDB baada ya ushindi wa mabao 3-2, matokeo yaliyoibua maswali na mijadala mingi miongoni mwa wadau wa soka nchini.

Lakini soka lina tabia ya kutoa nafasi ya kulipiza kisasi haraka. Leo Yanga imepewa nafasi hiyo. Hakuna nafasi ya kufanya makosa tena. Hakuna nafasi ya kuangalia nyuma. Ni mechi ya kupigania alama tatu, heshima ya timu na kuendelea kuongoza mbio za ubingwa.

Wananchi wanasubiri majibu kutoka kwa nyota wao uwanjani. Je, Yanga itasimama imara na kuonyesha kwa nini ni mabingwa watetezi? Au Azam FC itaendelea kuwa mwiba kwa Wananchi?

Majibu yote yatapatikana ndani ya dakika 90 za moto katika Uwanja wa New Amaan Complex.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’