Matchday; Yanga vs Azam Fc, NBC PL, Juni 24

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jun 2026
Matchday; Yanga vs Azam Fc, NBC PL, Juni 24

Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo mzunguuko w 28 ambapo saa 10 jioni timu zote 16 zitakuwa viwanjani kusaka alama tatu muhimu. Ni wiki ya lala salama, wiki ya kufunga hesabu za ligi kuu ya NBC msimu huu 2025/26. 

Mabingwa watetezi Yanga wako visiwani Zanzibar wakikabiliwa na kibarua kizito mbele ya Azam Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa New Amaan Complex.

Ni mechi inayokutanisha miamba ambao wametoka kumenyana siku tatu zilizopita kwenye nusu fainali ya kombe la CRDB Yanga ikikubali kipigo cha mabao 3-2 katika mchezo uliopigwa kwa dakika 120.

Presha iko juu, ukiangalia msimamo wa ligi tofauti alama mbili tu kati ya Yanga na Simba inayofuata kwenye nafasi ya pili. Ni wazi makosa yoyote kwa Yanga yanaweza kuwanufasha watani zao Simba katika mechi hizi za lala salama.

Ndio maana mchezo dhidi ya Azam Fc leo una umuhimu wa kipekee kwa sababu unaweza kubadili hali ya msimamo wa ligi hasa ikitokea Yanga wakapoteza.

Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa haina mbadala wa matokeo mazuri zaidi ya ushindi. Pamoja na kuwa matokeo ya sare bado yatawaweka kileleni mwa msimamo wa ligi lakini ni wazi yataongeza presha kuelekea mechi mbili za mwisho dhidi ya TRA United na JKT Tanzania.

Kocha Mkuu wa Yanga AbdiHamid Moalin amekiri mchezo wa leo hautakuwa mwepesi lakini jambo la uhakika ni kuwa vijana wake wako tayari na wanakwenda ukipambania nembo ya Yanga ili kuhakikisha wanashinda mchezo huo na kuhakikisha wanatetea taji la ligi kuu kwa msimu wa tano na kuandika historia mpya ya mafanikio kwa kizazi hiki.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’