Mkwasa asisitiza, Yanga haitashiriki Kagame Cup

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jun 2018
Mkwasa asisitiza, Yanga haitashiriki Kagame Cup
Juzi baada ya Yanga kuandika barua ya kujitoa kushiriki mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati yanayotambulika kama CECAFA Kagame Cup, Rais wa TFF Wallace Karia aliipa Yanga saa 48 kutengua barua hiyo kwa kuwa sababu walizokuwa wametoa hazikuwa na mashiko.

Leo Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesisitiza kuwa Yanga haitashiriki michuano hiyo kutokana na sababu walizozianisha awali lakini pia akaongeza kuwa klabu hiyo ina wachezaji saba tu.

"Baada ya kufanya tathmini tumebaini tuna wachezaji saba tu ambao wana mikataba iliyo hai huku kikosi chetu cha pili (Yanga B) kikiwa mkoani Dodoma kushiriki michuano ya Uhai Cup," amesema Mkwasa.

"Kwa sasa tuko kwenye mchakato wa kuimarisha timu yetu ikiwa ni pamoja na kuhuisha mikataba ya wachezaji ambayo imemalizika na kusajili wachezaji wapya."

"Tumewapa ruhusa wachezaji wako majumbani kwao. Tutawaita baada ya kukamilisha michakato muhimu kuanza maandalizi ya michuano ya kombe la Shirikisho."

Yanga itacheza na Gor Mahia Julai 18, 2018 huko nchini Kenya kisha kurudiana nayo jijini Dar es salaam Julai 29 kwenye michezo ya kombe la Shirikisho.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’