Buba anahesabu siku Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jun 2026
Buba anahesabu siku Yanga

Inaelezwa klabu ya Yanga haina mpango wa kuendelea na winga Buba Jammeh na ataondoka mwishoni mwa msimu.

Yanga ilimsajili Buba akitokea Angola kwenye dirisha dogo kwa mapendekezo ya kocha Pedro Goncalves hata hivyo nyota huyo raia wa Gambia ameshindwa kuthibitisha makali yake.

Kabla ya kujiunga na Yanga, Buba aliitumikia Interclube katika mechi saba zote zikiwa za Ligi Kuu Angola na kufunga bao moja, akiwa ni miongoni mwa nyota waliotabiriwa makubwa ingawa mambo yamekuwa tofauti.

Taarifa zaidi zimebainisha kuwa nyota huyo huenda akarejea Angola akitajwa kujiunga na klabu ya C.D. Primeiro de Agosto.

Yanga imejipanga kufanya maboresho makubwa ya kikosi pale dirisha la usajili litakapofunguliwa mwezi ujao ili kurejesha makali yao.

Msimu huu umekuwa mgumu kwa Yanga kutokana na changamoto walizokutana nazo kwenye usajili ambapo nyota wengi wapya waliosajiliwa msimu uliopita wameshindwa kuleta ushindani na kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Yanga inalazimika kutumia wachezaji wake walewale walioipa mafanikio katika misimu miwili au nyuma na kupelekea changamoto ya kikosi kuwa finyu.

Hali hiyo wakati mwingine imepelekea fatiki kwa wachezaji na kuonekana baadhi ya mechi wakitumia uzoefu kupata ushindi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’