Kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome ameweka wazi changamoto ya majeraha yaliyomsumbua kwa muda mrefu msimu huu akicheza baadhi ya mechi akiwa na maumivu makali.
Profesa huyo wa mpira amesema sasa ameimarika na yuko tayari kuipambania Yanga katika mechi zilizobaki kuhitimisha msimu huu.
Pacome jana alifunga bao la kwanza la Yanga kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate na kuwasaidia Wananchi kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Baada ya kufunga bao hilo Pacome alionyesha ishara ya shukrani akiieleza kwa mashabiki ambao wameendelea kumuunga mkono
“Ishara ile ni kuwashukuru mashabiki wa Yanga ambao wameweza kunivumilia katika kipindi kigumu. Nilicheza nikiwa na maumivu kwenye goti kwa kipindi kirefu kidogo lakini mara zote wamekuwa pamoja na mimi hata ninapokuwa katika nyakati ngumu uwanjani."
"Goli dhidi ya Fountain Gate ni muhimu sana kwangu katika wakati huu tunapoelekea mwisho wa Msimu."
"Najiskia vizuri sasa na niko tayari kuwapa mashabiki wetu kile wanachokitarajia kutoka kwetu. Waje kwa wingi uwanjani kutusapoti kwenye mechi hizi za mwisho,” alisema Pacome