Jana baada ya kufunga bao la pili kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Fountain Gate, mshambuliaji Laurindo Aurellio 'Depu' alikwenda moja kwa moja kushangilia na mashabiki.
Depu hakuchukua uamuzi huo kwa bahati mbaya, ni katika kutambua mchango wa mashabiki hao ambao wengi walitoa maoni yao mitandaoni wakitaka mshambuliaji huyo apatiwe muda zaidi wa kucheza kwenye kikosi cha kwanza.
Zilikuwa nyakati nzuri kwake kwani hakuwaangusha mashabiki akifunga bao muhimu ambalo unaweza kusema liliihakikishia Yanga kuondoka na alama tatu katika mchezo huo.
Depu alifunga bao lake la 7 msimu huu likiwa ni bao la 12 anafunga kwenye mashindano yote. Ikumbukwe Depu alitua Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo.
Wakati kuklwa na taarifa Yanga kuongeza mshambuliaji wa kigeni, ni wazi uongozi utalazimika kubadili maamuzi kama mpango wa mshambuliaji huyo ni kuchukua nafasi ya Depu.
Depu bado anaonekana kuwakosha mashabiki na wengi wanatamani kuona anaendelea kuwatumikia Wananchi msimu ujao