Shoo za Okello, Mudathiri kuendelea Arusha leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jun 2026
Shoo za Okello, Mudathiri kuendelea Arusha leo?

Ni saa chache kutoka sasa Yanga itashuka uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuikabili Fountain Gate katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.

Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na dhamira moja tu, kusaka ushindi ili iweze kurejea kwenye nafasi yake juu ya msimamo. Wananchi watashuka dimbani wakiwa na silaha zao zote katika mchezo huo.

Kiungo kiraka Mudathir Yahya ni miongoni mwa wachezaji wanaobeba matumaini ya Wananchi kutokana na mwenendo wake mzuri wa mechi za karibuni.

Mudathir anashika nafasi ya nne katika orodha ya vinara wa mabao ligi kuu ya NBC msimu huu akiwa na mabao 9 kama ilivyo kwa Prince Dube.

Feisal Salum 'Fei Toto' anaongoza mbio hizo akiwa na mabao 14 huku Mossi Ndumumwe wa Singida BS akiwa nafasi ya pili na mabao 12.

Star Boy Allan Okello anashika nafasi ya tatu akiwa ameweka kambani mabao 11.

Pengine leo Okello anaweza kuendeleza kasi yake ya kuzifumania nyavu baada ya kutofunga kwenye mchezo uliopita.

Baada ya kuonyesha kiwango kizuri dakika chache alizocheza kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mashujaa Fc, mshambuliaji Laurindo Aurelio 'Depu' leo huenda akapata nafasi ya kuanza kuwakabili Fountain Gate.

Depu na Dube leo bila ya kujali nani anaanza, watakuwa na kazi ya kuhakikisha nyavu za Fountain Gate hazitoki salama na kuwahakikisha Wananchi alama tatu muhimu.

Endapo Yanga itashinda mchezo wa leo basi itakuwa imepunguza presha kwani itarejea kileleni huku sasa ikisalia na mechi nyingine tatu za kuhakikisha ubingwa wa tano mfululizo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’