Kamwe awaita Wananchi kwa wingi Sheikh Amri Abeid

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jun 2026
Kamwe awaita Wananchi kwa wingi Sheikh Amri Abeid

Kikosi cha Yanga kiko mkoani Arusha ambapo leo watakamilisha maandalizi yao kuelekea mchezo dhidi ya Fountain Gate ambao utapigwa kesho Alhamisi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Wananchi wako kwenye msako wa ubingwa wa tano mfululizo, ushindani ukiwa mkali katika mechi hizi za lala salama.

Hivyo katika mchezo huo, alama tatu kwa Wananchi zitawafanya wakaribie kukamilisha malengo ingawa bado kutakuwa na mechi tatu ngumu za kuhitimisha.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki na wanachama wa timu hiyo mkoani Arusha kujitokeza kwa wingi dimba la Sheikh Amri Abeid kuiongezea hamasa timu yao.

Kamwe amesema katika mechi hizi za mwishoni jukumu la mapambano ya alama tatu sio la wachezaji pekee, kila mwanayanga anapaswa kushiriki kwa mashabiki kwenda kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu yao.

Fountain Gate imebadilika tangu ujio wa kocha Freddy Felix Minziro licha ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Azam Fc katika dimba la Sheikh Amri Abeid.

Hata hivyo licha ya ugumu wa mchezo huo, Yanga haitakuwa na mpango mwingine wa matokeo zaidi ya ushindi..

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’