Nahodha wa makombe awapa ujumbe Wananchi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jun 2026
Nahodha wa makombe awapa ujumbe Wananchi

Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amewataka mashabiki na wanachama wa timu hiyo kuhakikisha wanaunga mkono timu yao kwenye kila hatua katika mechi zilizobaki ili kuhakikisha wanamaliza msimu kwa nguvu na kutetea taji lao la ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo.

Juzi Mwamnyeto aliiongoza Yanga kupata ushindi muhimu wa mabao 2-0 dhidi ya Mashujaa Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Baada ya mchezo huo, Yanga imebakiwa na mechi nne ambazo kama watashinda zote au kushinda tatu na kutoa sare moja, watajihakikishia ubingwa kwa msimu wa tano mfululizo

“Natambua mechi nne zilizosalia siyo nyepesi, lakini kadri tunavyoshinda kama tulivyoshinda dhidi ya Mashujaa ndivyo tunavyozidi kusogea karibu na malengo yetu, jambo la msingi naendelea kuwasisitiza mashabiki walianza na sisi msimu kwa nguvu na wamalize na sisi kwa nguvu ileile"

“Kazi yetu wachezaji ni kuhakikisha tunawapa mashabiki furaha, ikitokea matokeo hayajawa mazuri basi inakuwa ni bahati mbaya, hivyo tunazidi kujipanga na kujiweka sawa ili tumalize kwa ushindi mechi zilizosalia,” alisema Mwamnyeto

Kikosi cha Yanga kimeendelea mkoani Arusha tayari kwa mchezo unaofuata dhidi ya Fountain Gate ambao utapigwa Alhamisi, Juni 18 uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Baada ya mchezo huo Yanga itahamishia nguvu kwenye nusu fainali ya kombe la CRDB dhidi ya Azam Fc mchezo utakaopigwa Juni 21 uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
2h ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
14h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
18h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
23h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’