Moalin aweka imani kwa Dube, Depu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Jun 2026
Moalin aweka imani kwa Dube, Depu

Kocha Mkuu wa Yanga Abdihamid Moalin ana matumaini makubwa kwa washambuliaji wake Prince Dube na Laurindo Aurelio 'Depu' kuwa watafanya vizuri kwenye mechi zilizobaki msimu huu baada ya kuwa na wakati mzuri walipokuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa.

Dube na Depu wamepitisha kipindi kirefu bila ya kuzifumania nyavu Dube akiweka kituo kwenye mabao 9 huku Depu akisimamia kwenye mabao sita.

Wakati wa mapumziko ya kalenda ya FIFA, Dube alielekea Zimbabwe kwenye majukumu ya timu ya Taifa akiifungia timu hiyo bao pekee la ushindi kwenye mchezo dhidi ya India.

Depu nae akiitumikia Angola, akafunga na kutoa pasi ya bao kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Afrika ya Kati.

Moalin amesema mabao waliyofunga kwenye mechi hizo za Kimataifa yatakuwa msaada mkubwa kwao kurejesha fomu yao kwenye kuzifumania nyavu.

“Ni hatua nzuri tumeona ndio wameanza kufunga, ukiwa kocha au mtu unayeipenda klabu hii hakika utafurahia kitu cha namna hii, nadhani sasa ni wakati mzuri watarudi klabuni wakiwa na morali tena umeifungia timu yako ya taifa”

“Watarudi wakiwa wanajiamini sasa, tutaendelea kuwapa nafasi kama ambavyo ilikuwa kabla kwa kuwa ni washambuliaji wetu na tunawaamini, unajua kwenye soka nyakati kama hizi ni kawaida kuna wakati unarudi chini na hili halidumu linapita na unarudi kufanya vizuri."

“Tuna mechi ngumu tano zimesalia kumaliza msimu tunafurahia kila mchezaji amerudi salama na wamefanya vizuri,” alisema Moalin

Yanga tayari iko mkoani Kigoma kuikabili Mashujaa Fc katika mchezo utakaopigwa Jumamosi, Juni 13 uwanja wa Lake Tanganyika

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’