Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ameikumbusha Bodi ya ligi kutoa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya NBC kwa mwezi May 2026.
Kiungo mshambuliaji wa Yanga Allan Okello ni mmoja wa wachezaji wanaopigiwa chapuo ya kushinda tuzo hiyo kutokana na takwimu bora za mwezi May.
Okello alifunga mabao 9 na kutoa pasi moja ya bao akiwazidi Clatous Chama wa Simba aliyefuunga mabao 5 na kutoa pasi 4 za mabao na Feisal Salum wa Azam Fc aliyefunga mabao 7 na kutoa pasi moja ya bao.
Kamwe anaamini Okello anastahili kushinda tuzo hiyo. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Kamwe ameandika ujumbe huu;
"Najua katikati hapa mambo yalikuwa mengi kidogo .. Hivyo kwa unyenyekevu mkubwa naomba kuwakumbusha BODI YA LIGI kuwa Yanga tunasubiri Tuzo ya STAR BOY ya mchezaji bora wa mwezi wa 5," aliandika Kamwe