Miloud aondoka Al Ittihad

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Jun 2026
Miloud aondoka Al Ittihad

Kocha wa zamani wa Yanga Miloud Hamdi ameondoka klabu ya Al Ittihad ya Misri baada ya msimu kufika tamati.

Baada ya kuondoka Yanga mwishoni mwa msimu uliopita, Hamdi alijiunga na Ismaily ya Misri na baadae kutua Al Ittihad.

Licha ya Al Ittihad kuhitaji kuendelea nae, kocha huyo amegoma kuongeza mkataba akihitaji changamoto mpya.

Msimu uliopita Miloud aliongoza benchi la ufundi la Yanga na kuweka rekodi ya kushinda mataji matano katika msimu ambao Yanga iliongozwa na makocha watatu ambao ni Miguel Gamondi, Sead Ramovic na yeye.

Alitua baada ya kuondoka Ramovic akiiongoza Yanga kwa mafanikio makubwa hadi mwisho wa msimu akishirikiana ya Abdihamid Moallin.

Ukiwauliza mashabiki wengi wa Yanga ni kocha gani wangependa arejee tena kuongoza benchi la ufundi kuelekea msimu ujao? Miloud anaweza kupata kura nyingi.

Miloud, Nasreddine Nabi na Sead Ramovic wote wako sokoni wakiwa hawana timu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’