Dala anatua Julai

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Jun 2026
Dala anatua Julai

Katika dirisha dogo Yanga ilifanya jitihada kubwa za kumpata winga wa Kimataifa wa Angola, Gelson Dala ambaye anaitumikia klabu ya Al Wakrah ya Qatar.

Mpango wa Yanga ilikuwa kuwasajili Laurindo Aurelio 'Depu' na Dala lakini walifanikiwa kumnasa Depu pekee.

Baada ya kukwama kumpata Dala, dakika za lala salama kuelekea kufungwa dirisha dogo, Wananchi wakafanikiwa kumsajili Buba Jammeh yakiwa ni mapendekezo ya kocha aliyeondoka Pedro Goncalves.

Goncalves aliwataka Depu na Dala kwa sababu ni wachezaji ambao alifanya nao kazi kwa mafanikio wakati akiinoa timu ya Taifa ya Angola.

Sasa mpango wa Yanga kumnasa Dala bado uko palepale na kuna uwezekano mkubwa akajiunga na mabingwa hao wa nchi kwenye dirisha kubwa litakalofunguliwa mwezi ujao.

Yanga na Dala walishafikia makubaliano kilichokwamisha mpango wa kutua dirisha dogo ni mchakato wa uhamisho wake kutoka klabu yake ya Al Wakrah ambayo kwa wakati huo haikuwa tayari kumuachia.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’