Baada ya Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuthibitisha mamlaka za soka nchini Morocco kusitisha mechi za kirafiki za mataifa mbalimbali zilizokuwa zipigwe nchni humo katika kipindi hiki cha mapumziko ya kalenda ya FIFA, kikosi cha Stars kinarejea nchini ambapo wachezaji watajiunga na timu zao.
Hii ni habari njema kwa Yanga kwani sasaa itakuwa na sehemu kubwa ya kikosi chake wakati huu wa maandalizi ya mechi za mwishoni mwa msimu.
Nyota wa Yanga ambao walikuwa kwenye kikosi cha Stars ni Nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto, Ibrahim Bacca na Mudathir Yahya.
Stars ilitarajiwa kucheza mechi za kirafiki dhidi ya Rwanda na Uganda huku Shirikisho la soka Uganda nalo likithibitisha kurejea kwa kikosi chao nchini humo.
Allan Okello alikuwa sehemu ya kikosi cha Uganda Cranes nae akirejea kuendelea na majukumu yake kwenye kikosi cha Yanga.
Mshambuliaji Prince Dube nae tayari amemaliza majukumu yake Zimbwabwe huku mlinda lango Djigui Diarra akitarajiwa kuitumikia nchi yake kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Irani.