Vipi arudi nyumbani?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Jun 2026
Vipi arudi nyumbani?

Kiungo Khalid Aucho yuko ukingoni mwa mkataba wake na klabu ya Singida Black Stars.

Baada ya msimu huu kufika tamati, Aucho atakuwa mchezaji huru akikamilisha mkataba wake wa mwaka mmoja.

Unaweza kusema tangu kuondoka kwa Aucho kwenye kikosi cha Yanga, pengo lake halikuzibika.

Yanga ilimsajili Moussa Balla Conte ambaye alishindwa kupenya kwenye kikosi cha kwanza na kupelekea mabingwa hao wa nchi kumtoa kwa mkopo kwenye usajili wa dirisha dogo huku wakimchukua kwa mkopo Mohamed Damaro 'Ngosha' kutoka Singida BS.

Katika kikosi cha Yanga Duke Abuya kwa sasa ndiye mchezaji tegemeo eneo la kiungo cha ukabaji akisaidiana na Damaro ambaye hata hivyo kadi za mara kwa mara zinamfanya akosekane mara kwa mara kikosini.

Ni wazi Yanga itarejea sokoni kusaka kiungo mkabaji na jina la Aucho ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa.

Aucho aliondoka Yanga baada ya makubaliano ya kimkataba kushindwa kufikiwa. Alihitaji mkataba wa miaka miwili huku Yanga ikiwa tayari kumpa mkataba wa mwaka mmoja.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’