Yanga Princess inamaliza msimu kinyonge

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 May 2026
Yanga Princess inamaliza msimu kinyonge

Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) inaelekea ukingoni huku Yanga Princess ikiendelea kusuasua baada ya leo kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya JKT Queens katika mchezo uliopigwa uwanja wa Isamuhyo.

JKT Queens walitangulia kufunga na Yanga Princess ikasawazisha kupitia Jeanine Mukandayisenga.

Ni mchezo wa nne mfululizo Yanga Princess inakosa ushindi ikipoteza mechi mbili na sare mbili.

Imekusanya alama 44 ikiwa nafasi ya pili alama moja mbele ya JKT Queens inayoshika nafasi ya tatu. Hata hivyo JKT Queens wana mchezo mmoja wa kiporo.

Tayari mbio za ubingwa zimefika tamati kwani Simba Queens wametwaa ubingwa baada ya ushindi dhidi ya Mashujaa Queens wakifikisha alama 56.

Msimu huu Yanga Princess ilianza vyema msimu lakini unaweza kusema baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Simba Queens ni kama bundi aliingia mitaa ya Jangwani.

Bila shaka maboresho zaidi yatafanyika pale dirisha la usajili litakapofunguliwa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
15h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’