FT : Yanga 3-1 Namungo Fc, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 May 2026
FT : Yanga 3-1 Namungo Fc, NBC PL

Shoo za Star Boy Allan Okello zimeendelea uwanja wa KMC Complex leo akiingoza Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.

Duke Abuya aliifungia Yanga la mapema dakika ya 26 kupitia shambulizi la kushitukiza kabla ya Namungo Fc kusawazisha kupitia Hassan Kabunda. Hadi mapumziko mzani ulikuwa sawa matokeo yakiwa sare ya bao 1-1.

Kipindi cha pili kilikuwa cha Okello alifunga bao la pili dakika ya 53 akimalizia mpira uliotemwa na mlinda lango wa Namungo Fc baada ya krosi ya Dube.

Wakati Namungo Fc wakitafuta bao la kusawazisha, alikuwa ni Okello tena kwa mara nyingine akifunga ndani ya 18 dakika ya 84 baada ya kumhadaa mlinzi wa Namungo.

Hilo lilikuwa bao la 11 kwa Okello sasa akiwa nyuma ya kinara wa mabao Feisal Salum aliyefunga mabao 12.

Ni rekodi kwa Okello kwani sasa amefunga katika mechi ya tano mfululizo akifunga mabao mawili katika mechi nne mfululizo. Mabao 9 ameyafunga katika mechi tano tu!

Wananchi wamerejea kileleni mwa msimamo wa ligi sasa wakifikisha alama 60 baada ya mechi 25.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’