Nahodha wa Yanga Bakari Mwamnyeto amewapa soma mashabiki wa Yanga juu ya umuhimu wa kuwaunga mkono wachezaji wao katika nyakati hizi ili kuhakikisha wanakuwa imara katika kuipambania timu yao ili kutetea ubingwa.
Baada ya kukosekana kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania, Mwamnyeto alirejea kikosini juzi kwenye ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Singida BS akiingia kuchukua nafasi ya Frank Assink.
Aidha Mwamnyeto pia ameeleza sababu iliyopelekea aombe kupumzika hasa baada ya matukio yaliyojitokeza kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji.
"Niliomba nipumzike kwa sababu Mzee wangu yupo hapa na anaumwa kwahiyo niliomba nipumzike nimuombee dua na familia maana alikuwa anaenda kufanyiwa operation. Hiyo ndio sababu ya kutocheza mechi ile (JKT Tanzania). "
"Yanga ni wachezaji na wachezaji ndio sisi hapa kwahiyo ukimtolea maneno machafu mchezaji unamvunja moyo ila kwa upande wangu mimi nishazoea hayo maneno lakini ukimwambia mchezaji mwingine mdogo kama Ninju au Casemiro hataweza kucheza mpira, atavunjika moyo na atashuka chini zaidi."
"Wananchi ndio mashabiki wetu na hii ndio timu yao, mimi nawapenda na wao wananipenda kwahiyo tushikamane katika hizi mechi 6 tuweze kutetea ubingwa wetu," alisema Mwamnyeto