Matchday; Yanga vs Singida BS, NBC PL, May 22

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 May 2026
Matchday; Yanga vs Singida BS, NBC PL, May 22

Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga watashuka uwanja wa KMC Complex kuikabili Singida BS katika mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali.

Wananchi wataingia kwenye mchezo huo huku wakifahamu wanahitaji matokeo ya aina moja tu, ushindi ili kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi.

Ndio! hakuna tena nafasi ya kufanya makosa, njia pekee ya Yanga kutetea taji la ligi kuu ni kushinda kila mchezo unaokuja mbele.

Hautakuwa mchezo mwepesi kwani hata Singida BS nao wako kwenye vita ya kuwania nafasi nne za juu ili washiriki michuano ya CAF msimu ujao.

Ikumbukwe Singida BS tayari wametupwa nje katika michuano ya kombe la Shirikisho (CRDB) hivyo nafasi pekee iliyobaki kwao ni ligi kuu.

Yanga imepata muda wa kutosha kujiandaa na mchezo huo hivyo matarajio ya mashabiki ni kuona timu yao ikichukua alama tatu katika mchezo huo mgumu.

Wananchi watashuka dimba la KMC Complex wakiwa na kikosi kamili kuikabili Singida BS katika mchezo ambao haitashangaza kuona mashabiki wa Simba wakijitokeza kwa wingi kuwaunga mkono Singida BS wakiamini matokeo mazuri kwa Singida BS ni faida kwao pia.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’