Kauli ya Rais TFF yawashangaza wengi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Jun 2018
Kauli ya Rais TFF yawashangaza wengi
Baada ya Yanga kuandika barua ya kujitoa kwenye mashindano ya CECAFA Kagame Cup, Shirikisho la soka Tanzani (TFF) limethibitisha kupokea barua hiyo.

Rais wa Shirikisho hilo Wallace Karia ameipa Yanga saa 48 kusitisha uamuzi wake kulingana na taarifa zilizoandikwa na baadhi ya magazeti ya leo.

Licha ya Yanga kutoa sababu zake za msingi zilizopelekea wajitoe, Karia amesema hazina mashiko kwa kuwa hata Gor Mahia inayoshiriki michuano ya kombe la Shirikisho ambayo itacheza na Yanga mchezo unaofuata, inashiriki mashindano haya.

Jambo la kushangaza hapa ni jinsi TFF inavyojaribu kuilazimisha Yanga ishiriki mashindano hayo kama vile hakuna timu nyingine.

Kila timu inaangalia maslahi yake, kushiriki kwa Gor Mahia haiwezi kuwa sababu kwa Yanga kushiriki pia.

Hata mashindano ya SportPesa Super Cup hayawezi kufananishwa na haya ya Kagame kwa kuwa yale yanafahamika.

Timu zote zinazodhaminiwa na kampuni ya SportPesa ni lazima zishiriki kulingana na mikataba yao.

Mashindano haya ya Kagame 'yamezuka' tu hayamo katika kalenda za nchini husika.

Kwa kuwa hayakupangwa mapema yamekuwa kama michezo ya kirafiki na hayatambuliwi na FIFA. Michuano muhimu inayotambuliwa na FIFA yote imesimama kupisha kombe la dunia.

Wapo wanao-hoji vigezo vilivyotumika kuzipata timu shiriki mwaka huu, basi na vitumike kumpata mbadala wa Yanga.

Mchecheto huu walioingia TFF baada ya Yanga kujitoa unadhihirisha dhamira ya waandaaji wa mashindano haya ni maslahi zaidi.

Wanafahamu Yanga ni moja ya timu zinazobeba mashindano hayo, kujitoa kwao kutafanya mashindano yakose msisimko.

Upo uwezekano mkubwa baada ya muda huo uliotolewa na Karia kupita Yanga itatangazwa kufungiwa kushiriki mashindano yajayo kwa miaka kadhaa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
15h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’