Mabingwa watetezi michuano ya kombe la Shirikisho la CRDB Yanga leo wako tena uwanjani kuisaka tiketi ya nusu fainali ya michuano hiyo pale watakapoikabili JKT Tanzania katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Isamuhyo, Mbweni jijini Dar es salaam.
Yanga ndio mabingwa wa michuano hiyo kwa misimu minne iliyopita, wana dakika 90 za kuisaka nufu fainali ya sita mfululizo.
Hii ni mechi muhimu kwa Yanga wakihitaji ushindi ili kurejesha furaha ya mashabiki wao baada ya kupoteza mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji.
Yanga imeweka malengo ya kutetea mataji yote mawili yaliyobaki yaani ligi kuu na kombe la CRDB.
Ni wazi hautakuwa mchezo mwepesi hasa ikizingatiwa JKT Tanzania wamejipambanua kuwa timu ngumu hasa wanapocheza katika uwanja wao wa Isamuhyo.
Yanga bado haijafanikiwa kupata ushindi katika mechi zote walizocheza katika uwanja huo zote zikimalizika kwa sare.
Hata hivyo mchezo wa leo ni lazima mshindi apatikane, dakika 90 zikimalizika kwa sare, mikwaju ya penati itatumika.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa 12:30 jioni..