Lile jambo kubwa linalosubiriwa kwa hamu ya mashabiki na Wanachama wa Yanga sasa linakwenda kutimia Makao Makuu, Jangwani jijini Dar es salaam.
Leo Yanga na GSM watasaini mkataba wa ujenzi wa uwanja wa kisasa katika eneo la Jangwani.
Mkuu wa mkoani wa Dar es salaam Mh Albert Chalamila ndiye mgeni rasmi kwenye tukio hilo la kihistoria.
Wengi walidhani viongozi wa Yanga wanafanya 'siasa' kwenye suala la ujenzi wa uwanja lakini sasa ni rasmi hakuna maneno mengi tena, ni utekelezaji kwa vitendo.
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said aliwaahidi Wanayanga kuwa atahakikisha Yanga inapata uwanja kabla ya kuondoka kwenye majukumu ya kuiongoza Yanga.
Leo ni hatua muhimu kuelekea kukamilika kwa ahadi hiyo ambayo awali wengi waliibeza.

ADVERTISE HERE