Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mabingwa watetezi Yanga wako mkoani Singida kuikabili Dodoma Jiji. Ni katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Airtel Mtipa.
Ni mchezo mwingine muhimu kwa Yanga kuzisaka alama tatu muhimu ili kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa.
Hata hivyo vijana wa kocha Abdihamid Moalin watahitaji kuwa kwenye ubora wao ili kupata ushindi mbele ya Dodoma Jiji inayoonekana kuimarika zaidi kwenye mechi za karibuni.
Wakati Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo uliopita, Dodoma Jiji walipata alama moja mkoani Mwanza mbele ya Pamba Jiji.
Habari njema kwa Yanga leo ni kurejea kwa kiungo Mudathir Yahya aliyemaliza adhabu ya kufungiwa mechi tatu.
Aidha katika mchezo huo huenda mlinzi wa kushoto Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' akarejea kikosini baada ya kupona majeraha yaliyomfanya akose mechi nne zilizopita kwenye mashindano yote.
Mchezo unatarajiwa kupigwa saa 10 jioni..