Kamwe aibana BMT tuzo ya klabu bora ya mwaka 2025

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 May 2026
Kamwe aibana BMT tuzo ya klabu bora ya mwaka 2025

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe ameendelea kuibua mjadala kuhusu tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka 2025 iliyotolewa na Baraza la Michezo la Taifa kwa Simba SC.

Kamwe amehoji vigezo vilivyotumika kumpata mshindi wa tuzo hiyo, hasa ikielezwa kuwa sababu kubwa ya Simba kushinda ni kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup).

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Kamwe alikumbusha namna mwaka 2023 Yanga ilivyotwaa tuzo hiyo kwa kuzingatia mafanikio kadhaa makubwa yaliyopatikana ndani na nje ya nchi.

Kwa mujibu wa Kamwe, mwaka huo Yanga ilipewa tuzo kutokana na:

  • Kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC)
  • Kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara
  • Kushinda Kombe la Shirikisho la Azam

Kamwe ameonyesha kushangazwa na kile alichodai kuwa ni mabadiliko ya ghafla ya vigezo vya utoaji wa tuzo hizo.

“Mwaka 2023 sababu zilielezwa wazi kabisa mbele ya wadau wote. Leo tunaambiwa hatuna elimu na hatujui vigezo,” alihoji Kamwe.

Aidha, Kamwe amesema hali hiyo inaonyesha kuwa mafanikio ya ndani kama ubingwa wa ligi na makombe ya nyumbani hayapewi uzito mkubwa mbele ya mafanikio ya kufika hatua za mwisho katika michuano ya kimataifa.

Kwa mtazamo wake, ujumbe unaotolewa na BMT ni kwamba hata timu ikitwaa makombe mengi ya ndani, bado hayana thamani kubwa mbele ya timu iliyofika fainali ya mashindano ya CAF.

Msimu uliopita Yanga ilitwaa mataji yote ya ndani yaani Ngao ya Jamii, Ligi Kuu, kombe la Mapinduzi, kombe la Muungano na kombe la CRDB lakini mataji hayo hayajatosha kwa Wananchi kushinda tuzo hiyo mbele ya watani zao Simba waliomaliza msimu bilaa taji lolote zaidi ya kucheza fainali ya CAFCC

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’