FT : Yanga 3-0 Coastal Union, NBC PL, May 09

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 May 2026
FT : Yanga 3-0 Coastal Union, NBC PL, May 09

Mabingwa watetezi ligi kuu ya NBC Yanga wameendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kuichapa Coastal Union mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex.

Wananchi walionyesha dhamira ya kuzihitaji alama tatu mapema tu Allan Okello akifunga bao la kwanza dakika ya 18 akimalizia kazi nzuri ya Prince Dube.

Licha ya kufungwa bao la mapema Coastal Union walihimili mikiki mikiki ya Wananchi na kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili Yanga ilirejea na kasi ya kusaka bao la pili huku Coastal Union nao wakiinuka kusaka bao la kusawazisha.

Hata hivyo ni Yanga iliyoongeza bao la pili kupitia kwa Okello kwa mara ya pili dakika ya 62 akipiga shuti kali akimalizia mpira wa krosi kutoka kwa Pacome.

Bao la tatu liliwekwa kimiani na Maxi Nzengeli dakika ya 75 pasi ikitoka kwa Okello ambaye aliondoka na tuzo ya nyota wa mchezo baada ya kuhusika kwenye mabao yote matatu.

Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe alama 54 sasa ikiongoza ligi kwa tofauti ya alama nane.

Aidha msimu huu Yanga sasa imefikisha mabao 50 huku ikiwa imeruhusu mabao matano.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’