Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo raundi ya 22 ambapo mabingwa watetezi Yanga watakuwa nyumbani uwanja KMC Complex kuikabili Coastal Union.
Ni mechi nyingine muhimu kwa Wananchi kuwania alama tatu ili kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa kwa msimu wa tano mfululizo.
Haitakuwa mechi rahisi, Coastal Union haijawahi kuwa mpinzani mwepesi hasa inapokuatana na Yanga.
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana mkoani Dodoma kwenye mchezo wa duru ya kwanza, Yanga ililazimika kusubiri hadi dakika ya 88 kuibuka na ushindi kwa bao la Prince Dube.
Wakati huu ligi inaelekea ukingoni, kila alama tatu zina umuhimu mkubwa hakuna nafasi ya kufanya makosa.
Mkufunzi wa Yanga Abdihamid Moalin amewaahidi Wananchi leo watarajie burudani ya aina yake kutoka kwa timu yao na muhimu zaidi kuchukua alama tatu mbele ya Coastal Union.
Baada ya Azam Fc kuchapwa na TRA United jana, Ynga ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo kwenye ligi msimu huu.
Wananchi wanashuka KMC Complex leo sio kuzisaka alama tatu tu, bali pia kuendeleza rekodi yao ya kipekee wakiwa wamecheza mechi 40 bila kupoteza ligi kuu