Licha ya ugumu wa ratiba tutaendelea kupambana - Mshery

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 May 2026
Licha ya ugumu wa ratiba tutaendelea kupambana - Mshery

Mlinda lango wa Yanga Aboutwalib Mshery amesema licha ya kukabiliwa na ratiba ngumu ya kucheza mechi mfululizo, wachezaji wataendelea kupambana ili kuhakikisha wanafikia malengo ya kutetea taji la ligi kuu.

Kesho Jumamosi Yanga itakuwa uwanja wa KMC Complex kumenyana na Coastal Union ikiwa ni siku tatu baada ya mchezo dhidi ya KMC ambao Wananchi waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mshery amesema wanaendelea kujiimarisha chini ya makocha wao huku wakiwa na matumaini ya kufanya vyema katika mechi zilizobaki.

“Ratiba imekuwa ngumu. Mechi zimefuatana sana. Tumekuwa na wakati mzuri licha ya matokeo magumu kwa baadhi ya michezo. Jambo zuri ni kuwa bado tupo kileleni mwa ligi."

"Waalimu waliopo kwa sasa wanatambua nini kinahitajika. Tunaendelea kupokea maagizo na maelekezo yao. Tuna matumaini makubwa ya kufanya vizuri kutokana na mshikamano ambayo upo katika timu yetu”

“Kila mwalimu anayekuja hapa anakuja na mbinu zake. Kwetu Moallin sio mgeni kwa sababu aliwahi kuwapo hapa. Hapa ni nyumbani kwake. Moallin anaifahamu Yanga vizuri sana."

"Hakuna mabadiliko makubwa kwenye timu yetu ambayo yanaweza kumpa wakati mgumu kutimiza majukumu yake kwa sasa. Tunaendelea kufanya kile ambacho anakitaka na tuna imani kubwa kwenye safari hii pamoja nae,” alisema Mshery

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’