Jana Afisa Habari wa KMC Khalid Chukuchuku alisikika akisema kuwa leo lengo lao ni kuirejesha rasmi Simba kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu kwa kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya Yanga.
Yaani KMC hawaingii uwanja wa KMC Complex wakiwa lengo la kutafuta alama tatu ili wajinusuru na hatari ya kuteremka daraja, bali kupambana ili kuirejesha Simba kwenye mbio za ubingwa.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ameonyesha kusikitishwa na kauli hiyo akibainisha kuwa kama ingetolewa na timu nyingine dhidi ya Simba pingine mjadala ungekuwa mkali zaidi.
Hata hivyo ni kauli ambayo inaweza kuwaponza KMC na wakakutana na hasira ya Wananchi. Yaani Simba wenyewe wameshindwa kuifunga Yanga tena katika uwanja wao, waarajie KMC wawasaidie!
Ni wazi leo Yanga itashuka dimba la KMC huku wakifahamu wanacheza dhidi ya timu iliyopewa jukumu la kuirudisha Simba kwenye mbio za ubingwa.