Sikuwa na mechi nzuri, nimejifunza kutokana na makosa - Mwenda

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 May 2026
Sikuwa na mechi nzuri, nimejifunza kutokana na makosa - Mwenda

Beki wa Yanga Israel Mwenda amekiri leo makosa yake yameigharimu timu bao la kwanza huku akiwaomba radhi mashabiki na wanachama kutokana tukio hilo.

Mapema dakika ya pili Mwenda alipoteza mpira eneo la hatari na kuwapa nafasi Simba kufunga bao la kwanza.

Tukio hilo ni kama lilimuondoa Mwenda mchezoni ambapo kocha Pedro Goncalves alilazimika kumfaanyia mabadiliko wakati wa mapumziko nafasi yake ikichukuliwa na Yao Kouassi.

"Sikuwa na siku nzuri kazini, nimekosea na kuigharimu TEAM nimewaangusha wachezaji wenzangu na mashabiki."

"Hakuna kisingizio na ntawajibika na kupokea lawama zote kwa mchezo wa leo. Wananchi hamkustaili kuona juhudi zenu na sapoti zikiishia bila furaha."

"Nimejifunza kwa makosa na ntapambana zaidi kurudi nikiwa bora kuliko leo," aliandika ujumbe Mwenda kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.

Hata hivyo Yanga ilifanikiwa kusawazisha mabao yote na mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Yanga inaendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa ligi ikifkikisha alama 48, tofauti ikibaki alama 5.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’