Hakuna muda wa lawama, dabi nyingine ni Jumapili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Apr 2026
Hakuna muda wa lawama, dabi nyingine ni Jumapili

Kupoteza mchezo wa fainali kombe la Muungano dhidi ya Simba ni matokeo yaliyowaumiza sana mashabiki wa Yanga kutokana na upinzani wa asili uliopo baina ya timu hizo.

Matokeo hayo yasingekuwa na maumivu makali kama Yanga ingepoteza dhidi ya timu nyingine na sio Simba.

Lakini ulikuwa mchezo wa fainali ambao lazima mshindi apatikane, wakati huu bahati imekuwa upande wa Simba. Mapema msimu huu Yanga ilitwaa Ngao ya Jamii kwa kuifunga Simba bao 1-0, ndivyo matokeo ya mpira yalivyo.

Jana Yanga ilitawala mchezo kwa muda mwingi hasa kipindi cha kwanza na kuwa na matukio mazuri zaidi ya kufunga kwenye kpindi cha pili.

Tukio moja tu dakika za lala salama kwenye 'extra time' ndilo lililoingharimu Yanga na kupoteza mchezo huo wakifungwa kupitia mkwaju wa penati baada ya Edmund John kumkwatua Clatous Chama katika jitihada za kuondoa mpira eneo la hatari.

Wachezaji wa Yanga walipambana kwa muda wote, wakitengeneza nafasi bora zaidi, unaweza kusema pia bahati haikuwa upande wao.

Kuna dakika nyingine 90 muhimu katika siku tatu zijazo, mchezo wa May 03 dhidi ya Simba unamaana kubwa kwa Yanga katika mkakati wa kutetea taji la ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo.

Yanga inahitaji kushinda mchezo huu sio kulipa kisasi tu, bali pia kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa.

Wananchi wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama 5 ushindi dhidi ya Simba utaongeza gap hilo na kufikia alama 8. Katika mazingira hayo Yanga itakuwa imewasha taa ya kijani kuelekea ubingwa wa 32.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’