Kwa mara ya kwanza katika mchezo wa dabi ya Kariakoo, kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua hakuwa na mechi nzuri jana.
Katika mchezo wa fainali kombe la Muungano ambao mashabiki walikuwa na matumaini makubwa na urejeo wake hasa baada ya kukosa mchezo uliopita, mambo yalikuwa magumu kwake.
Pengine ni ulinzi mkali ambao aliwekewa na Simba lakini pia zipo nyakati angeweza kufanya vyema zaidi lakini alichelewa katika kufanya maamuzi.
Ni mchezo ambao Pacome anapaswa kusahau haraka na kuhakikisha anafanyia kazi baadhi ya changamoto ili siku ya Jumapili afanye kile kilichotarajiwa.
Baada ya kupoteza kombe la Muungano, Yanga sasa inapaswa kupambana kutetea mataji mawili yaliyobaki, Ligi Kuu na kombe la CRDB.
Ushindi katika mchezo dhidi ya Simba siku ya Jumapili utaiweka Yanga katika nafasi nzuri ya kutetea taji la ligi kuu sasa wakiongoza msimamo kwa tofauti ya alama 5.