Yanga imetinga nusu fainali ya kombe la Muungano baada ya kuichapa Muembe Makumbi mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa New Aman Complex visiwani Zanzibar.
Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Yanga walitawala mchezo huo tangu mwanzo wakifunga mabao yao kupitia kwa Prince Dube liyepachika mabao mawili, Shekhan Khamis huku bao moja likiwa la kujifunga Muembe Makumbi.
Ulikuwa mchezo wa upande mmoja kwa muda mwingi Muembe Makumbi wakishindwa kabisa kuipenya ngome ya Yanga wala kumpa changamoto mlinda lango Djigui Diarra.
Kwa upande wa tuzo binafsi, Shekhan Khamis alingβara na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi, huku Mudathir Yahya akiondoka na tuzo ya nidhamu kutokana na mwenendo wake mzuri uwanjani.
Yanga sasa inasubiri mshindi wa mchezo mwingine wa robo fainali kati ya KVZ dhidi ya Azam Fc utakaopigwa Jumatano.
