Yanga imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kuifumua Mbeya City mabao 6-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex.
Wananchi walihitaji dakika 45 za kipindi cha kwanza kumaliza mchezo huo baada ya kufunga mabao matano hadi wakati wa mapumziko.
Baada ya kukosekana kwenye baadhi ya mechi kutokana na majeruhi, mshambuliaji Prince Dube amerejea kikamilifu kwenye kikosi cha kwanza na ilikuwa siku nzuri kwake kurejea akifunga mabao mawili.
Alifungua kalamu ya mabao kwa kufunga bao la kwanza na pia akifunga bao la sita mwishoni mwa kipindi cha kwanza.
Mabao mengine yalifungwa na Pacome Zouzoua aliyefunga mabao mawili huku Maxi Nzengeli na Mohamed Hussein wakifunga mengine mawili.
Kiungo mshambuliaji Allan Okello ameendeleza kasi yake ya kupika mabao leo akiongeza asisti mbili kwa mabao ya Zimbwe Jr na Maxi
Yanga ilitawala mchezo huo kwa muda mwingi wakiwabana Mbeya City ambao walikosa kabisa mbinu ya kuipenya ngome ya mabingwa hao watetezi iliyokuwa chini ya nahodha Bakari Mwamnyeto huku langoni akianza Hussein Masalanga.
Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe alama 47 kileleni na kuongeza gap la pointi kuwa alama 8.



