Okello atuma ujumbe mzito kuelekea mchezo dhidi ya TMA Stars

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Apr 2026
Okello atuma ujumbe mzito kuelekea mchezo dhidi ya TMA Stars

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Allan Okello amesema litakuwa kosa kubwa kuwadharau wapinzani wao TMA Stars wanaokutana nao kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya robo fainali kombe la CRDB ambao utapigwa kesho Jumamosi uwanja wa KMC Complex.

Okello amewataka wachezaji wenzake kuhakikisha wanaendeleza kiwango bora walichoonyesha kwenye michezo iliyopita ya ligi kuu, akiamini wana kila sababu ya kushinda mchezo huo kutokana na ubora wa kikosi chao.

Okello amesema TMA Stars hawana cha kupoteza kwenye mchezo huo lakini itakuwa habari kubwa endapo Yanga itakosa ushindi na kuondoshwa katika michuano hiyo.

"Ndugu zetu hawana cha kupoteza katika mchezo wa kesho. Endapo sisi tutapoteza bila shaka itakwenda kuwa habari kubwa. Ni wajibu wetu wachezaji kubaki kwenye malengo ya msingi."

"Hatupaswi kuwabeza hata kidogo. Mpira wa miguu unahitaji kuwa na heshima kwa kila mpinzani. Nguvu tunayotumia dhidi ya wapinzani wa ligi kuu inapaswa kutumika vile vile ili kuonesha utofauti”

“Nina matumaini makubwa kama tutaendelea na morali ya mchezo uliopita basi tutapata ushindi wa kishindo. Wachezaji tunapaswa kuwa watulivu uwanjani na kufuata maelekezo ya waalimu wetu."

"Tuna wajibu wa kuipigania nembo ya Yanga. Ukifanya kosa moja tu kwenye mchezo wa mtoano inaweza kubadilish historia. Hii sio ligi. Ninawahakikishia wananchi kuwa tutamaliza kila kitu ndani ya dakika 90,” alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’