Kikosi cha Yanga kimerejea salama jijini Dar es salaam wakitokea Mwanza ambako jana walichapa Pamba Jiji mabao 3-0 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba.
Baada ya kurejea, Wananchi watakuwa na mapumziko ya siku moja kabla ya kurejea mazoezini hapo kesho kukamilisha maandalizi ya mchezo wa hatua ya 16 bora kombe la CRDB dhidi ya TMA utakaopigwa uwanja wa KMC Complex.





ADVERTISE HERE