Wananchi Yanga wametakata uwanja wa CCM Kirumba Mwanza wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Pamba Jiji katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.
Ulikuwa mchezo ambao Yanga ilionyesha dhamira ya kusaka ushindi mapema tu dakika ya nane Mudathir Yahya akifunga bao la mapema akimalizia pasi ya Allan Okello aliyekuwa kwenye kiwango bora leo.
Okello na Mudathir wakashirikiana tena kuiandikia Yanga bao la pili dakika ya 34 kwa mara nyingine pasi ikitoka kwa Okello.
Bao la tatu liliwekwa kambani na Maxi Nzengeli dakika ya 67 ni yule yule tena Stars Boy Okello aliyetoa pasi ya bao hilo.
Ushindi huo unaifanya Yanga kuwa klabu ya kwanza kupata ushindi dhidi ya Pamba Jiji katika uwanja wa CCM Kirumba msimu huu.
Lakini pia ni kipigo cha pili Pamba Jiji wanakutana nacho kutoka kwa Yanga mechi ya duru ya kwanza pia walichapwa mabao 3-0
Ni alama tatu muhimu kwa Yanga ambazo zinawafanya wazidi kupanua wigo wa uongozi wao juu ya msimamo wakifikisha alama 44.



