Mwenda awaalika mashabiki CCM Kirumba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Apr 2026
Mwenda awaalika mashabiki CCM Kirumba

Mlinzi wa Yanga Israel Mwenda amesema wachezaji wanatambua ugumu wa mchezo ulio mbele yao dhidi ya Pamba Jiji utakaopigwa kesho katika uwanja wa CCM Kirumba.

Mwenda amesema wachezaji wamejiandaa kupambana kwa nguvu zote wakitambua hiyo ndio njia pekee kwao kushinda mchezo huo.

Mwenda amewaalika mashabiki wa Yanga jijini Mwanza na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi uwanja wa CCM Kirumba kuwaunga mkono katika mchezo huo.

“Kwa niaba ya wachezaji wenzangu, tunatambua umuhimu wa mchezo wa kesho pamoja na ubora wa mpinzani tutakayekutana naye."

"Mchezo wa kesho utahitaji mapambano makubwa na kila mmoja wetu analitambua hilo. Tumerejea katika ari ya ushindi na tunakusudia kuendeleza mwenendo huo katika michezo yetu."

"Tunawaalika Wananchi wa Mwanza na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kutupa sapoti. Tunawahakikishia kuwa tutapambana kwa nguvu zote ili waondoke wakiwa na furaha,” alisema

Mwenda amesisitiza kuwa wachezaji wa Yanga hawana presha yoyote kuelekea mchezo huo kwa sababu wanafahamu ukiwa klabu ya Yanga unapaswa kuwa tayari kukabiliana na mazingira ya aina yoyote.

“Hatuna presha kuelekea mchezo wa kesho. Unapocheza katika klabu ya Young Africans unapaswa kuwa tayari na uzoefu wa kukabiliana na mazingira ya aina yoyote bila kuwa na presha."

"Kama wachezaji, tumejielekeza zaidi katika umakini na maandalizi sahihi kuelekea mchezo huo, tukitambua umuhimu wake na wajibu tulionao uwanjani.”

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’